Mwamuzi wa kati Israel Nkong'o kutoka hapa nchini,
anatarajiwa kushika kipyenga kwenye mechi ya kombe la Ligi
ya Mabingwa Afrika kati ya Zesco United ya Zambia na
AS Kaloum ya Guinea utakaofanyika Machi 13 huko nchini
Zambia.
Nkong'o atakuwa akisaidiwa na Watanzania wenzake John
Kanyenye na Josephat Bilali huku mezani akiwepo Waziri
Sheha wakati Kamisaa wa mchezo huo akiwa ni Elvin Mshani
kutoka Afrika Kusini.
Wakati huohuo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),
limetangaza viingilio kwa ajili ya mechi ya Yanga na Simba
utakaochezwa Jumapili hii jijini.
Jukwaa la VIP A bei ya tiketi ni shilingi 40,000, VIP B silingi
30,000, VIP C elfu 20, 000 wakati viti vya rangi ya kijani na
bluu bei ya tiketi itakuwa ni shilingi elfu saba.
Kizuguto pia alitaja vituo vitakavyotumika kuuzia tiketi kuwa ni
Oil Com Buguruni, Big Bon Kariakoo, Stendi ya daladala
Makumbusho, TFF Karume, Dar Live Mbagala na
Mgahawa wa Steers Posta mpya.
TFF imewataka mashabiki wa soka watakaojitokeza uwanjani
siku hiyo kutoingia na chupa za maji, mabegi au silaha uwanjani
hapo kwani ulinzi utakuwa ni wa uhakika huku pia idadi ya
magari yatakayoingia uwanjani siku hiyo yakitakiwa kutozidi
mia.
Waamuzi wa Tanzania waula Afrika
Info Post