Breaking News
Loading...
Monday, 23 April 2018

Info Post


Nyota wa Liverpool Sadio Mane ametoa kiasi cha fedha cha pauni 200,000 ili kusaidia kujenga shule ya kisasa huko nchini Senegal.

Shule hiyo ni ya sekondari na itajengwa katika mji anaotokea mama yake, Bambaly uliopo Senegali kusini.
Hundi ya fedha ilikabidhiwa na mjomba wake Sana Toure kwenye sherehe.
.
" Ninawaambia vijana wadogo ambao wanataka kuwa Mane,Balde....elimu ni muhimu sana, ndiyo itakayokufanya kuwa na ' Career' nzuri, " alisema Mane kwenye hotuba yake iliyosomwa na Mjomba wake.

Baada ya kupokea fedha hiyo ambayo ni sawa na shillingi za Kitanzania  637,462,000 wananchi waliohudhuria walimwombea dua Mane azidi kufanikiwa.

Hii si mara ya kwanza kwa Mane kuisaidia jamii yake, katika miaka iliyopita,Mane alitoa ufadhili kwa wanafunzi waliokuwa na vigezo vya kwenda chuo, alitoa pikipiki kwa vijana kwa ajili ya kufanyia biashara, pia amewahi kutoa magari ya wagonjwa katika Hospitali na misaada mingine kwa wanajamii.