Breaking News
Loading...
Monday, 23 April 2018

Info Post

Singida United imetinga kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho Azam Fedaration Cup kwa kuifunga JKT Tanzania bao 2-1 kwenye mechi ya nusu fainali iliyochezwa leo kwenye Uwanja wa Namfua mkoani Singida.

Singida United sasa itamenyana na Mtibwa Sugar kwenye Fainali za Kombe la Shirikisho la Azam itakayochezwa Juni 2 mwaka huu kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid uliopo mkoani Arusha.

Mabao ya Singida United yamefungwa na Tafadzwa Kutinyu dakika ya 54,98 na bao la JKT Tanzania limefungwa na Hassan Matelema katika dakika ya 38 ya mchezo.