Breaking News
Loading...
Sunday, 22 April 2018

Info Post

Magoli kutoka kwa Olivier Giroud na Alvaro Morata yametosha kuipeleka Chelsea katika fainali ya kombe la FA baada ya kuitungua Southampton 2-0 dimba la Wembley.

Chelsea sasa watakabiliana dhidi ya Manchester United katika dimba hilo hilo la Wembley mwezi ujao .

Antonio Conte na Jose Mourinho msimu huu wamekutana mara mbili kila mmoja akishinda mara moja na mechi ya fainali itakuwa nafasi ya kocha mmoja wao kumfunga mwenzake mara nyingi.

Na bingwa wa kombe hili atakutana na Manchester City katika mechi ya ngao ya jamii mwanzoni mwa msimu ujao.