Breaking News
Loading...
Wednesday, 25 April 2018

Info Post

Matumaini ya Alex Oxlade-Chamberlain kusafiri na timu ya taifa ya Uingereza yameingiwa na hofu baada ya kiungo huyo kubebwa na kutolewa nje kwenye mechi ya nusu fainali ya UEFA dhidi ya AS Roma jana Usiku.

Kiungo huyo wa kimataifa wa Uingereza imeonakana kwamba ameumia goti lake la kulia akiwa anawania mpira na beki wa Roma Aleksandar Kolarov katika dakika ya 18 na kupatiwa matibabu ya muda mrefu uwanjani.

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp ana wasiwasi kwamba kiungo huyo  ameumia vibaya na huku kocha wa Uingereza Gareth Southgate anatarajiwa kutaja kikosi chake cha awali cha wachezaji 35 mwezi Mei tarehe 14 na nafasi ya Oxlade-Chamberlain ipo mashakani.

. " Hatujui kikamilifu lakini kama idara ya madaktari ina wasiwasi tena bila vipimo , unaweza kuona kwamba ni ngumu sana."

. " Msimu unakaribia kuisha , kwahiyo haionekani nzuri kwake ."

. " Mimi ni mtu chanya sana na bado nina matumaini kwamba inaonekana mbaya lakini sio mbaya sana , ngoja tuone."

. " Tumempoteza mchezaji mzuri sana leo usiku, kwahiyo sio taarifa nzuri .