Santi Carzola ameonekana akifanya mazoezi katika dimba la Emirates kuelekea mechi ya nusu fainali ya kombe la Europa dhidi ya Atletico Madrid.
Carzola amekuwa nje ya dimba tangu Oktoba 2016 baada ya kuumia kifundo cha mguu na hatimaye kulazimika kufanyiwa upasuaji mara 10
Na ilifikia hatua kwamba kukatwa mguu wake ilikuwa inafikiriwa na madaktari.
Hata hivyo kwa taarifa nzuri kwa Gunners Carzola ameonekana katika dimba la Emirates akifanya mazoezi na akifanya vipindi vya mazoezi na kocha Shaf Fosythe.
Bado Arsenal hawajasema lini atarejea rasmi dimbani huku mkataba wake ukifikia tamati mwishoni mwa msimu huu.