Breaking News
Loading...
Thursday, 26 April 2018

Info Post


Ikiwa kombe la dunia lipo kwenye kona  meneja wa Sweden ametoa kauli nzito akisema hatoenda na ' Living Legend' wa Sweden Zlatan Ibrahimovic kombe la dunia litakaloanza kutimua vumbi Urusi mwezi wa sita mwaka huu.

Zlatan alitangaza kustaafu soka la kimataifa baada ya fainali za Euro 2016 lakini hivi karibuni alisikika akisema anataka kwenda kucheza kombe la dunia kwani hakuna Kombe la Dunia bila Zlatan.

Taarifa iliyochapwa katika ukurasa wa Instagram wa timu ya Taifa ya Sweden imesema kuwa: 'Ujumbe wa mwisho, Zlatan hatacheza kombe la Dunia .'
.
Meneja wa timu hiyo Lars Richt kupitia taarifa hiyo amesema kuwa : ' Niliongea na Zlatan siku ya jumanne. Amesema hajabadili maamuzi yake kuhusu (kustaafu) timu ya Taifa . '
.
Zlatan alikuwa anatibu majeraha ya goti akiwa na United kabla ya kutua LA Galaxy ambapo ameonekana kurudi kwenye kiwango chake ambacho tumekizoea ikiwa mechi yake ya kwanza na Galaxy akifunga mabao mawili.

Sweden walishiriki kombe la dunia mara ya mwisho 2006 wakishindwa kufuzu ya 2010 na 2014 hivyo pengine uzoefu wa mtu kama Zlatan ambaye amecheza World Cup za 2002 na 2006 ungehitajika Urusi.