Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi (Kamati ya Saa 72) ya Bodi ya Ligi katika kikao chake kilichopita taarifa na matukio mbalimbali na kufanya
Mchezaji Tafadzwa Kutinyu wa Singida United amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na kufanya vitendo vyenye kuonyesha imani za ushirikina katika mechi hiyo iliyochezwa Aprili 6, 2018 kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida.
Katika mchezo huo, Kutinyu alichukua taulo la kipa wa Mtibwa Sugar na kulirusha jukwaani kwa washabiki wa Singida United ambao waliondoka nalo. Adhabu dhidi yake imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 37(7) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Wachezaji.