Wakiwa wachezaji 10 uwanjani Atletico Madrid wamefanikiwa kupata goli la ugenini na kuilazimisha Arsenal sare ya 1-1 ndani ya Emirates katika mechi ya kwanza ya nusu fainali ya kombe la Europa.
Arsenal sasa watalazimika kufunga angalau goli katika mechi ya marudiano ili watinge fainali wiki ijayo mjini Madrid dimba la Wanda Metropolitano.
Atletico Madrid wanahitaji sare ya 0-0 au hata ushindi kabisa kutinga fainali itakayopigwa jijini Lyon mwezo ujao
Goli la Arsenal limewekwa kambani na Alex Lacazette na Tony Griezmann akisawazisha kwa Atletico.
Kwingineko nchini Ufaransa , Marseille wamepata ushindi mzuri wa 2-0 wakiwa kwao kwa kuwatungua RedBull Salzburg ya Austria . Magoli ya Clinton Nje na Florian Thauvin yametosha kuipa Marseillr mtaji mzuri kuelekea mechi ya marudiano wiki ijayo.