Bila kuwa katika kiwango cha juu, Real Madrid walipata nafasi nne tu za kupiga golini na mawili yameingia wavuni kutoka kwa Marcelo na Marco Asensio na kuipa Madrid uongozi wa magoli 2-1 .
Joshua Kimmich ndio mfungaji wa goli pekee la Bayern Munich ambao walitengeneza nafasi za kutosha kufunga zaidi hata ya magoli manne katika dakika 90 zote.
Siku sita zijazo watarudiana dimba la Bernabeu kutafuta mshindi wa kucheza jijini Kyiv fainali ya kombe la UEFA.
Hakika kila siku tunashuhudia mpira ukitupa matokeo ya kikatili sana.