Breaking News
Loading...
Tuesday, 24 April 2018

Info Post

Mawili kutoka kwa Mo Salah, mawili ya Bobby Firmino na moja kutoka Sadio Mane yameipa Liverpool uongozi wa magoli 5-2 dhidi ya AS Roma katika dimba la Anfield mechi ya kwanza ya nusu Fainali Ligi ya Mabingwa.
.
Magoli ya Edin Dzeko na Diego Perotti yameipa Roma magoli mawili ya Ugenini.

Kwa matokeo haya AS Roma wanahitaji ushindi wa magoli matatu bila majibu ili kusonga mbele huku Liverpool wakihitaji sare tu au hata kufungwa magoli yasiyozidi mawili wataweza kutinga fainali.

Unadhani Roma anaweza kufanya kwa Liverpool kama alivyofanya kwa Barcelona ???