Breaking News
Loading...
Saturday, 14 April 2018

Info Post
 


Nathaniel Clyne na  Ragnar Klavan ni majina yatakayoungana na orodha ya wachezaji watakaokosa mchezo dhidi  AFC Bournemouth leo Jumamosi
Hata hivyo kocha Klopp ameeleza kuwa nahodha Jordan Henderson anarejea dimbani leo baada ya kukosa mchezo wao dhidi ya Manchester City Jumanne iliyopita kutokana na  kusimamishwa. Pia Roberto Firmino atakuwepo licha ya kuwa na tatizo dogo katika shingo. “kwa bahati mbaya , nafikiri , sio asilimia 100, kwamba Raggy anatatizo kidogo kwenye Misuli. Clyne huenda akawa nje, kwani alipata majeraha katika mazoezi baada ya mchezo dhidi ya City. Alisema Klopp
Kama Clyne na Klavan wanaondolewa katika kikosi hivyo itamlazimu kloop kuwavaa Bournemouth bila wachezaji wake 6 wa kikosi cha kwanza kwani pia anamkosa
Adam Lallana (misuli), Joel Matip (nyonga ),
Joe Gomez (Kifundo cha mguu ) na  Emre Can (mgongo ) .
Je kocha Eddie Howe atatumiaa pengo ilo la kukosekana kwa wachezaji 6 wa kikosi cha Liverpool kuweza kuwaadhibu ?