Zikiwa zimebaki dakika chache mechi kumalizika, Iddy Suleiman anawaliza watoto wa jangwani kwa kujitwisha kichwa na kuisawazishia Mbeya City dhdi ya Yanga SC na kufanya mechi kuisha sare ya 1-1 ndani ya dimba la Sokoine jijini Mbeya.
Yanga SC sasa wanakuwa na Pointi 48, Pointi 11 nyuma ya vinara Simba SC wenye pointi 59 huku simba akibakiza michezo 5 na Yanga akibakiza michezo 7 ligi kuisha.
Tarehe 29 /04 wikiendi ijayo ni Kariakoo Derby ambapo vilabu vyote viwili vimetoka kudondosha pointi ugenini ( lipuli 1-1 Simba na Mbeya 1-1 Yanga )