Mtendaji Mkuu wa Arsenal Ivan Gazidis - Mwanaume ambaye anahusika na kupendekeza kocha mpya kwa mmiliki Stan Kroenke anaamini kwamba Mikel Arteta ndio kocha ambaye anafaa kuvaa viatu vya Arsene Wenger, kwa mujibu wa taarifa kutoka Sky Sports.
Gazidis anaamini kwamba klabu inatakiwa kuwa ' jasiri ' katika mchakato wa kutafuta kocha mpya na anaamini kwamba licha ya Arteta kukosa uzoefu wa kuwa kocha mkuu , kiungo huyo wa zamani wa Arsenal ana sifa za kufanikiwa katika kazi hiyo.
Arteta ambaye aliwahi kuwa Nahodha wa Arsenal heshima yake inazidi kuwa kubwa kwa kocha mbunifu akifanya kazi pembeni na Pep Guardiola pale Manchester City.
Arsenal bado hawajasema lolote kuhusu taarifa hiyo lakini leo Jumatatu Gazidis aliongea na wafanyakazi 200 wa klabu hiyo pale Emirates kuwaelezea utaratibu gani utatumika kutafuta mrithi wa Wenger.
Gazidis pamoja na mkuu wa shughuli za mpira wa miguu Raul Sanllehi na Mkuu wa Kitengo cha Usajili Sven Mislintat, wiki hii wataanza mazungumzo na makocha wanaowahitaji.
Taarifa kutoka Sky Sports zinasema kwamba Sanllehi ambaye aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Michezo wa Barcelona anamtaka zaidi Luis Enrique kuchukua mikoba ya Wenger.
Na Mkuu wa kitengo cha usajili wa Arsenal , Sven Mislintat yeye angependa zaidi kocha mpya wa Arsenal awe kocha Julian Nagelsmann kutoka Hoffenheim au Domenico Tedesco kutoka Schalke.
- Gazidis --- anamtaka Arteta
.
.
- Sanllehi ----- anamtaka Enrique
.
.
- Sven Mislintat -- anamtaka Nagelsmann au Nagelsmann