Kocha msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa ameonesha kufurahia matokeo ya droo hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika ilivyopangwa na wao kucheza na timu jirani za Afrika Mashariki huku akidai wana nafasi kubwa ya kufanya vizuri
"Kitu kikubwa ambacho tunatakiwa kukifanya ni maandalizi mazuri na ya mapema, tukifanikiwa hilo kila kitu kitakuwa rahisi kwetu. Tumepangiwa na Gor Mahia na Rayons ni timu ambazo tunajuana vizuri, ligi zao tunaziona na ya kwetu wanaiangalia hivyo ni jukumu letu kufanyia kazi tu ubora wao na mapungufu yao,"
"Msimu uliopita tulitolewa na Waalgeria sasa cha kufanya hapo ni kuangalia kwa umakini tulikosea wapi na kitu gani cha kufanya ili tuweze kufanikiwa kuifunga USM Alger na sisi kusonga mbele zaidi."