Klabu ya Yanga imeamua kukata rufaa TFF kulalamikia mchezaji mmoja wa Mbeya City kuzidi Uwanjani.
Mwenyekiti wa Mashindano wa Wanajangwani hao Hussein Nyika, amesema kuwa wametuma malalamiko kufuatia mchezaji wa Mbeya City kuonekana Uwanjani wakiwa 11 badala ya 10 wakati mmoja wao alikuwa ameshatolewa nje ya Uwanja kwa kadi nyekundu.
Beki wa Mbeya City, Ramadhan Malima anadaiwa kuonekana Uwanjani wakati zikiwa zimebakia dakika takribani 6 mchezo kumalizika ilhali alikua ametolewa kwa kadi nyekundu.