Breaking News
Loading...
Sunday, 6 May 2018

Info Post

AC Milan wanataka kumsajili straika wa zamani wa Manchester City Edin Dzeko majira ya kiangazi, kwa mujibu wa taarifa kutoka Tuttosport.

Dzeko amekuwa na mafaniko mazuri ndani ya Roma kwa kuweka kambani mara 73 katika mechi 136, na Milan wanamtaka kuongoza safu yao ya ushambuliaji msimu ujao.

Taarifa zinasema kwamba miamba hiyo ya San Sirro inataka kumtumia Straika Carlos Bacca kama 'chambo' katika harakati zao za kumnasa Dzeko.

Bacca, 31 kwa sasa yupo kwa mkopo katika klabu ya Villarrea na klabu hiyo ya Hispania wana kipengele cha kumnunua moja kwa moja kwa thamani ya Euro Milioni 15.5 . Na ameripotiwa kutaka kubaki Hispania.