Breaking News
Loading...
Thursday, 10 May 2018

Info Post


Winga wa Barcelona aliye kwa mkopo nchini Uturuki, Arda Turan amefungiwa mechi 16 baada ya kumsukuma mwamuzi wa pembeni ( Linesmen) wikiendi iliyopita.

Turan mwenye umri wa miaka 31 aliruhusiwa kuhamia klabu ya Basaksehir mwezi Januari kwa uhamisho wa mkopo wa miaka miwili na nusu baada ya kushindwa kuonyesha kiwango kizuri ndani ya Camp Nou akitokea Atletico Madrid mwaka 2016.

Akisajiliwa kuongeza nguvu katika kikosi hiko ambacho kipo  kwenye harakati za kuwania kutwaa taji la Ligi ya Uturuki kwa mara ya kwanza katika Historia yao amecheza mechi 11 mpaka leo na kufunga magoli mawili.

Lakini katika sare ya 1-1 dhidi ya Sivasspor, Turan alikasirika baada ya timu yake kunyimwa mpira wa adhabu ndogo na hatimaye kumsukuma mwamuzi wa pembeni.

Mchezaji huyo alionyesha hasira sana na kumsukuma mwamuzi wa pembeni na kuondoka mahala hapo . Mwamuzi wa kati akamuonyesha kadi nyekundu , na Bodi ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka la Uturuki limemuunga mkono mwamuzi na kutoa kifungo cha muda mrefu zaidi katika Historia ya Soka la Uturuki.

Turan atakosa mechi mbili za mwisho za Ligi za klabu yake Basaksehir huku klabu yake ikiwa nyuma kwa Pointi mbili dhidi ya Vinara Galatasaray