Breaking News
Loading...
Thursday, 10 May 2018

Info Post

 DANIEL S.FUTE

*Inaendelea...* WAKATI umefika na muda ndio huu. Hapo jana niliweza kuelezea vyema kuhusu Uwanja wa Luzhniki, ambao ndio uwanja maalumu wa kufungua na kufunga fainali za Kombe la Dunia mwaka huu.

Leo ni vyema ni kaendelea na uwanja wa pili kati ya viwanja 12, ambavyo ni shiriki katika fainali hizi zinazotarajia kuanza mwezi Juni. Ni kujuze kwamba uwanja ambao nitauzungumzia leo ni uwanja wa pili baada ya Luzhniki katika uingizaji wa watu.

*Saint Petersburg*

Saint Petersburg ni Uwanja ambao upo katika kisiwa cha Krestovsky, ambapo kisiwa hicho kipo katika mji wa Saint Petersburg.

Uwanja huu upo chini ya umiliki wa klabu ya Zenit Saint-Petersburg ambayo inashiriki katika Ligi kuu ya Urusi. Shirikisho la Soka Dunia 'FIFA', lilifanya uchaguzi huu kulingana na uwezo na ubora wa uwanja huu ambao si tofauti sana na ule wa Luzhniki.

Mwaka 2007 uwanja wa Saint Petersburg uliweza kutanuliwa pitch na kufikia uwezo wa 105 * 68 m. Lakini baada ya hapo FIFA walipouteua uwanja huu kuwa utatumika kwa fainali za Kombe la Dunia, uliweza kuongezwa kutoka idadi ya kuingiza watu 56,196 hadi kufikia 67,000 wakati ulipokamilika mwaka 2017.

Uwanja huu unatarajiwa kuchezewa mechi saba tu katika fainali za Kombe la Dunia, mechi hizo ni:

★15 June 2018 17:00 – Morocco vs Iran – Group B

★19 June 2018 21:00 – Russia vs Egypt – Group A

★22 June 2018 15:00 – Brazil vs Costa Rica – Group E

★26 June 2018 21:00 – Nigeria vs Argentina – Group D

★3 July 2018 17:00 – 1F vs 2E – Round of 16

★10 July 2018 21:00 – W57 vs W58 – Semi Final

★14 July 2018 17:00 – L61 vs L62 – Third Place

Hizo ndizo mechi ambazo zitachezwa hapo Saint Petersburg, Usikose tena hapo kesho na muendelezo wa makala hii.