Breaking News
Loading...
Thursday, 10 May 2018

Info Post



Shirikisho la Soka barani Ulaya UEFA limethibitisha kwamba vilabu vinne vya juu vya ligi kuu ya soka ya Uingereza watafuzu moja kwa moja kucheza Ligi ya mabingwa Ulaya msimu ujao hata kama Liverpool watatwaa taji la UEFA na kumaliza nafasi ya tano.

Chelsea walitwaa taji hilo kwa mara ya kwanza mwaka 2012 lakini walimaliza nafasi ya sita katika ligi , na kufanya Tottenham waliomaliza nafasi ya nne kukosa nafasu ya kucheza mashindano ya UEFA.

UEFA wamesema," Mabingwa wa Ligi ya mabingwa Ulaya wanahakikishiwa nafasi ya hatua ya makundi , hata kama wakishindwa kufuzu kupitia ligi ya nyumbani katika nafasi stahili."
.
. " Upatikanaji wa nafasi hiyo haitoathiri wale waliomaliza nafasi nne za juu , na kwa kesi ya Liverpool , kama wakiwa mabingwa wa Ulaya , na wakishindwa kufuzu kupitia ligi ya nyumbani , basi washirika hao watawakilishwa na timu tano katika mashindano."
.
. " Na hao watakuwa, Bingwa wa UEFA, mshindi wa kwanza wa Ligi, wa pili, wa tatu na wa nne "