Ni Mnyamaaaaaaaaa ..!!!
Wekundu wa Msimbazi Simba SC rasmi wamekuwa Mabingwa wapya wa Ligi kuu ya soka ya Tanzania Bara msimu wa 2017/2018 baada ya Yanga SC kukubali kichapo cha 2-0 kutoka kwa Prisons ya Mbeya .
Simba SC wana pointi 65 ambazo haziwezi kufikiwa na Yanga SC hata akishinda mechi zake zote tano zilizobaki za msimu huu.
Sasa baada ya kuwa mabingwa Simba SC watakuwa na jukumu la kufukuzia rekodi ya kumaliza msimu wa Ligi bila kupoteza mechi hata moja ya Ligi.
Hongereza Simba, Wachezaji, Uongozi pamoja na Mashabiki kwa Ujumla.....Tukutane 2018/2019.