Breaking News
Loading...
Monday, 14 May 2018

Info Post


Mkono mmoja umemzuia Barcelona kumaliza ligi bila kupoteza mechi baada ya kutunguliwa kwa jumla ya magoli 5-4 dhidi ya Levante katika mechi ya La Liga.

Barcelona alikuwa amebakiza mechi mbili tu kumaliza ligi ya La Liga bila kupoteza mechi, mojawapo ilikuwa ya leo dhidi ya Levante lakini vijana hao wamemwagia ' Kitumbua Mchanga ' 
Wazungu wanasema ' No Messi, No Party '  leo mabingwa hao wa La Liga waliingia dimbani bila nyota wao Lionel Messi. Kwa jinsi mechi ilivyokuwa imefunguka ilikuwa inahitaji ' ukatili ' wa La Pulga mbele ya goli .

Mwanaume kutoka Levante E.Boateng amemtungua Ter Stegen mara tatu ( Hat Trick ) na Philipe Coutinho naye kafunga ' Hat Trick ' yake ya kwanza ndani ya Barca.