Breaking News
Loading...
Sunday, 6 May 2018

Info Post

Ndio maana ya El Classico wachezaji wakubwa wanaamua matokeo, Lionel Messi, Luis Suarez, Cristiano Ronaldo na Gareth Bale wote wamefunga magoli kufanya mechi kuisha 2-2 .

Mechi ya 35 zikibaki mechi tatu ligi kuisha Barcelona bado hawajapoteza mechi hata moja katika msimu huu wa La Liga wakicheza kipindi cha pili chote wakiwa pungufu baada ya Sergi Roberto kutolewa kwa kadi nyekundu.

Lionel Messi kafikisha magoli 33 kuelekea kutwaa Pichichi na pia amejiweka mahala
Pazuri kwa kutwaa kiatu cha dhahabu cha mfungaji bora wa bara la Ulaya akimpiku MO Salah kwa magoli mawili huku Salah akibaki na mechi moja Messi mechi tatu.