Mabingwa watetezi wa Ligi kuu ya Soka ya Tanzania Bara Yanga SC wameanza vibaya hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika baada ya kukubali kichapo cha 4-0 kutoka kwa USM Alger ya Algeria.
Yanga sc walisafiri kwenda Algeria bila ya wachezaji wake nyota takribani saba wakiwemo Ajibu , Shishimbi , Yondani.
Yanga sasa wamebaki na mechi 5 za kupata matokeo ili wapate nafasi ya kucheza robo fainali.