Fainal ya Asfc kufanyika leo jijini Arusha ikiwakutanisha timu ya Mtibwa Sugar kutokea mananungu turiani morogoro akikabiliana na Singida United ya jijini Singida kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha majila ya Saa Tisa mchana.
Hii ni Mara ya Kwanza Kwa Jiji za Arusha Kuwa Mwenyeji wa Fainali Kubwa Kwa Miaka ya hivi Karibuni hivyo inavutia Watazamaji wengi na Wapenzi wa Soka pamoja na Viongozi wa Serikali na Mpira wa Miguu.
TFF Mapema Ilitangaza Viingilio vya Mchezo huu Ambapo Kiingilio cha Chini ni 1000 Kwa Jukwaa C,2000 Kwa Jukwaa B na Jukwaa ambalo haliingizi Watazamaji Wasiozidi 500 litakuwa ni 10,000.
Kwa Mujibu wa Mujibu wa Viongozi wa Chama cha Soka Mkoani Arusha (ARFA) Uwanja huo una Uwezo wa Kuingiza Watazamaji 11,000 na tiketi za Mchezo Zinaanza Kuuzwa hii leo Nje ya Mageti ya Uwanja na Saa 2.00 Asubuhi Mageti yote yatakuwa wazi.